GET /api/v0.1/hansard/entries/826768/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 826768,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/826768/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kajiado CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. Janet Teiyaa",
    "speaker": {
        "id": 13239,
        "legal_name": "Janet Marania Teyiaa",
        "slug": "janet-marania-teyiaa"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nizungumze kwa Mjadala huu. Nashukuru Seneti sana kwa kutuletea mabadiliko haya kuhusu bunge zetu za kaunti. Tumeona mambo kadhaa yakitendeka katika bunge zetu za kaunti, mengi ambayo hayapendezi. Jambo la kwanza ambalo nataka kulizungumzia ni kumuondoa Spika kwenye kiti. Tumeona mambo mengi katika kaunti tofauti na mambo hayo hayajapendeza. Tunataka sheria ambayo inalinda spika akiwa kwenye kiti. Jambo jingine ni uajiri wa wafanyakazi katika bunge zetu za kaunti. Bunge zetu za kaunti mara nyingi hazitumii uwazi kuwaajiri wafanyakazi na hili ni jambo kubwa ambalo halipendezi watu katika kaunti zetu kwasababu hatuwachukui wafanyakazi kulingana na uwezo wao wa kutendakazi bali tunatumia njia kadhaa tofuti ambazo hazisaidii. Ni vizuri kama mtu ana uwezo na masomo yakutosha apewe kazi katika kaunti yake bila kuangalia rangi, kabila, chama ama mlango. Unajua kaunti nyingine zina milango na madirisha. Kwa hivyo, tukipata uwazi huo, kaunti zetu zitaendelea vizuri. Jambo lingine ni Ofisi ya Naibu wa Spika. Ni vizuri pia iwe na uwazi ili watu wajue kazi ya Naibu wa Spika. Isikuwe jina tu bali iwe ofisi inayoonekena. Naunga mkono uapishaji wa Wabunge wa Kaunti. Wanapaswa waapishwe siku ya kwanza ya bunge ili waweze kutendakazi yao kama vile Katiba yetu ilitarajia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}