GET /api/v0.1/hansard/entries/827293/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 827293,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/827293/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Mswada huu unalinda wananchi wasifanyiwe ubaguzi wa kidini, kijinsia au kitabaka. Kifungu 13, kinalinda watu kutokana na data yao kutimika kuwabagua kibinadamu, kidini, kirangi, kikabila na vingenevyo. Hapo nyuma hasa jamii ya Waisilamu, wale wanaotoka sehemu za Kaskazini Mashariki mwa Kenya wamefanyiwa ubaguzi na wakakusanywa pamoja na kuchunguzwa ilhali wengi wao hawakuwa wahalifu. Mswada huu unaweza kusaidia sana kuhakikisha ya kwamba haki za kibinadamu zinalindwa katika nchi ya Kenya. Mswada huu unazingatia pakubwa data isitumike kwa njia ambayo si sawa. Katika Kifungu cha 14, wanasema kwamba data ichukuliwe ikizingatia usiri wa mtu anayechukuliwa na vile vile pia isitumike kwa njia ambayo si ya kisheria. Usalama wa data umsezingatiwa katika Mswada huu. Unakwenda pakubwa kuhakikisha kwamba usalama unatekelezwa. Ningependa kujiunga na wenzangu ambao walizungumza awali. Kwa sasa nchi inapoteza raslimali nyingi kuagizia, kwa mfano, zile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}