GET /api/v0.1/hansard/entries/827298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 827298,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/827298/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ya watu binafsi na kuitumia kwa mambo yao ya biashara. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu kwa sababu utaenda pakubwa kuhakikisha kwamba data za raia wa Kenya na mashirika kadha wa kadha zitalindwa na kuhakikisha kwamba kuna usalama na uwazi zinavyokusanywa. Bw. Naibu Spika, kuna vipengee vya kuwahukumu wale ambao watapatikana na hatia. Najiunga na Seneta wa Migori kusema kwamba ile hukumu ambayo imepeanwa ni nyepesi kwa sababu matatizo ambayo yatatokea wakati data itatumika vibaya ni makubwa kulingana na vile ambavyo yule ameiiba ataitumia. Kuna haja ya kulinda data ya watoto na wale ambao hawajafikia umri wa miaka 18 kwa sababu data inaweza kutumika vibaya, hasa kwa wakati huu ambapo kuna visa vingi vya kutumika katika filamu chafu na mambo ya ngono kwa watoto ambao hawajatimia umri wa miaka 18. Kwa hivyo, ipo haja ya kuilinda kikamilifu na kuhakikisha kwamba data hii inalindwa. Nimefurahi pia kwamba kutakuwa na tume kuhakikisha kwamba hii sheria inatekelezwa kwa ukamilifu zaidi. Bw. Naibu Spika, kwa hayo mengi naunga mkono Mswada huu. Ni wakati mwafaka kuhakikisha kwamba umepitishwa. Nampongeza Sen. Abshiro kwa kuchangia pakubwa katika Mswada huu na pia kuleta mbele ya Seneti na kuhakikisha kwamba umesomwa na ukajadiliwa. Asante sana, Bw. Naibu Spika."
}