GET /api/v0.1/hansard/entries/830732/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 830732,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/830732/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Vilevile, ardhi haijawachwa kwa maana wakati mfumo wa elimu unabadilishwa, lazima pia ardhi iwe tofauti. Ni vyema Serikali kutunga sheria na vilevile mwongozo mwafaka na thabiti ambao unaweza kusaidia zile shule ambazo miaka ya 1960, 1970, 1980 na 1990 idadi ya watu ilikuwa chini. Sasa hivi, idadi hiyo imeongezeka. Yafaa Serikali itenge hela za kununua ardhi ya kupanua hizi shule badala ya kujenga shule nyingi. Zile shule za zamani zikipanuliwa, zitaweza kuwa na watoto wengi kuliko hapo mbeleni. Hoja hii imeletwa wakati mwafaka kwa maana kuna mambo mengi sana ambayo yamebadilika. Ni vyema kuwe na sheria na mwongozo kwa hizi shule na tujue mpangilio. Mwongozo utolewe kwamba shule ya msingi iwe na kiasi fulani cha ardhi, shule ya upili iwe na kiasi fulani cha ardhi. Juzi kulikuwa na matapeli wengine kule Mwatate ambao walisema wanataka kutujengea chuo kikuu kutoka Amerika kumbe wameshikana wanataka kuchukua ardhi. Walikuwa wanahitaji ekari 1000. Uzuri tuligundua hivyo. Ingekuwa vizuri wizara husika kutunga sheria kuhusu kiwango cha ardhi shule ya msingi, shule ya upili ama chuo kikuu zinahitaji. Vilevile, waangalie sana. Tukisema kuwa tuchukue ardhi yote kwa sababu ya mashule tukumbuke pia kuna zahanati na mambo mengine mengi yanayotakikana. Lazima tubadilishe mtindo. Kama tunajenga shule, tufikirie kuzijenga kama ghorofa ili shule zisichukue ardhi yote."
}