GET /api/v0.1/hansard/entries/830896/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 830896,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/830896/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "wengi waliulizwa kama wako na vyeti fulani vya kuonyesha ujuzi. Ikawa hawana vyeti vyovyote. Ni mafundi ambao wanatajika kwa jina vijijini lakini wakienda kujitafutia nafasi ya kujiendeleza, wanakuta hawawezi pata nafasi. Tunajua nchi yetu sana imekumbwa na umaskini, watu wetu mashinani wanachangamoto nyingi. Wengi katika vile vituo ambavyo vinaitwa TVET vilikuwa vimedharaulika sana mbeleni kwamba ni wale tu ambao wanakosa kufanikwa kuenda shule za upili lakini mafundi wengi tunaowajua hawana vyeti. Kwa hivyo, Hoja hii imekuja wakati sawa ili vijana wetu wapate kujiendeleza, mafundi wapate kujiendeleza kwa hali zao za maisha maanake ufundi wako nao. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Asante."
}