GET /api/v0.1/hansard/entries/832781/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 832781,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/832781/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ijapokuwa bodaboda zimeweza kurahisisha usafiri katika maeneo mengi nchini, kuna athari nyingi ambazo zimechibuka kutokana na biashara hii. Kwa mfano, wengi wanaoendesha bodaboda, hawana vibali rasmi vya Serikali vya kuwaruhusu kufnaya hivyo. Wengi wanaendesha bodaboda, bila ya kupata mafunzo yoyote ya uendeshaji wa boda boda hapa nchini. Vilevile, wengi wanaendesha bodaboda bila ya kuvaa vikinga kama vile kofia na reflector ambayo inaonyesha kwamba wao ni waendeshaji wa bodaboda. Bi. Spika wa Muda, katika hospitali nyingi, kumetengwa wodi maalum za kutibu wahasiriwa na majeruhi wa boda boda. Wengi wa wahasiriwa hao wamevunjika mikono, miguu na vichwa kubondeka. Ajali za bodaboda huarithiri sana uchumi wa nchi yetu. Mbali na hayo, waendeshaji boda boda pia huchukua sheria mikononi mwao. Wiki mbili zilizopita, walimuua kijana wa Chuo Kikuu cha Nairobi, katika eneo la Bamburi kule Mombasa. Kijana huyo alikuwa amekwenda na boda boda yake katika sehemu hiyo, lakini kwa bahati mbaya, akajaribu kuendesha bodaboda ambayo ilikuwa imeegezwa karibu na yake. Katika hali hiyo ya kuchanganyikiwa, waendeshaji boda boda wengine walidhani alikuwa mwizi, basi wakampiga na kumuua. Kijana huyo angehitimu masomo yake katika chuo hicho mwezi wa Disemba mwaka huu. Bi. Spika wa Muda, ukipatikana na waendeshaji wa boda boda mahali popopote kulingana nao umekosea hata kama wao ndio wenye makosa. Wao huchukua sheria mikononi mwao na wanaweza kufanya lolote, hasa barabarani. Wanaweza kuyahatarisha maisha yako na hata kukuua kutokana na tabia zao mbaya. Wao hawapendi kufuata sheria za barabarani. Bi. Spika wa Muda, waendeshaji boda boda wamekuwa tishio kubwa kwa wasichana wetu wa shule. Sehemu nyingi za mashambani na mjini ambapo wasichana wanapata shida ya usafiri kwenda shule au kutoka sehemu moja hadi nyingine, wanapata shida nyingi kutoka kwao. Wakati mwingine waendeshaji hawa huwapa wasichana wetu lifti na wakitoka hapo, inakuwa ni matatizo kwa wao na familia yao. Kwa mfano, wengi wa wasichana hupata maradhi ya yanayotokana na ngono za lazima kama vile ukimwi. Baadhi ya waendeshaji boda boda wameziletea jamii zetu majonzi na shida nyingi kutokana na tabia zao mbaya. Bi. Spika wa Muda, boda boda zimechangia pakubwa visa vya utovu wa nidhamu kwa wanafunzi wengi. Wanafunzi wengi wakipewa boda boda wakiwa wanaeza kuendesha, tayari wanaacha masomo yao ya shule na wanafuata biashara ya boda boda, wakati hana chochote cha kuweza kumsongeza mbele. Ni wakati muafaka sasa kuhakiksha kwamba, National Transport and Safety Authority (NTSA), wametoa sheria mwafaka, za kuhakikisha kwamba boda boda zinafuata sheria. Bi. Spika wa Muda, juzi tulikuwa nchini Rwanda ambapo waendeshaji boda boda hufuata sheria maalum. Utapata kila mwendeshaji wa boda boda na abiria wake wanavaa kofia na reflector migongoni kulingana na sheria. Kwa hivyo, ni wakati mwafaka kuhakikisha kwamba biashara ya boda boda imedhibitiwa hapa nchini. Ni lazima tuwe na sheria kali za kuhakikisha waendeshaji bodaboda na abiria wao wanasafirishwa kwa njia ya heshima na usalama."
}