GET /api/v0.1/hansard/entries/833668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 833668,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/833668/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa kutoa mwongozo wa kutoa malalamiko katika mabaraza ya kaunti zetu. Mswada huu umekuja katika wakati mwafaka kwa sababu tunaona kwamba Bunge za Kaunti zinaendelea kukua na kutatua matatizo ya wananchi katika Jamhuri ya Kenya. Kwa hivyo tukitoa mwongozo wa kupeleka malalamiko katika Bunge hizi, itawapa wananchi fursa ya kuweza kupeleka malalamiko yao bila ya kuwa na matatizo ya pesa ama ya kisheria ambayo mwananchi anaweza kushindwa kuyatatua kabla ya kufikisha malalamiko yale katika sehemu ambayo yanatakikana kutatuliwa. Mswada huu utaboresha uwezo wa mabaraza ya kaunti kuweza kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao. Tumeona kwamba, taasisi zinazo amua matatizo kama vile mahakama na mabaraza ya chifu, zimekwama kwa ajili ya mlumbiko wa matatizo. Kwa mfano, ukiangalia mahakama zetu hivi sasa zinalalamika kwamba majaji ni wachache na kesi zinazopelekwa ni nyingi. Kwa hivyo, fursa kama hii ikipewa mabaraza ya kaunti yataweza kurahisisha matatizo ya wananchi kwa sababu matatizo yao yatakuwa yanatatuliwa kwa haraka zaidi. Muda uliowekwa wa siku 60 ni mwafaka. Mwananchi ataweza kujua matatizo yake yameamuliwa vipi katika muda huol Mwongozo lazima uwe ni rahisi kwa mananchi kuuelewa. Kuna taasisi nyingi ambazo mwongozo wao si rahisi kuuwelewa. Kwa mfano, mahakama; mwongozo wake si rahisi kwa mwananchi kuuelewa. Kwa hivyo, kama hii ni sheria ya kusaidia mwananchi, lazima iwe na njia rahisi ya kuwezesha mwananchi kufikisha malalamiko yake mahali ambapo yatatatuliwa. Ningependekeza kwamba mwongozo utowe fursa ya mwananchi kueleza matatizo yake kwa njia ya maneno; yaani, oral presentation of the petition . Tungesema pia waruhusiwe kueleza katika lugha ya mama na iwe ni jukumu la karani wa kaunti ama bunge la kaunti kutafsiri kwa lugha ya kiingereza ama lugha ya Kiswahili ili wabunge wa kaunti waweze kulitatua tatizo lile. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}