GET /api/v0.1/hansard/entries/833669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 833669,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/833669/?format=api",
"text_counter": 288,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Japokuwa tunasema kwamba muongozo uwe rahisi, tukiangalia kifungu namba 3(k), kinasema kwamba ile sahihi ya mwenye kuleta malalamiko isiwe imebandikwa. Kwa hakika, hilo ni jambo ambalo litapinga hilo swala ambalo linasema kwamba muongozo uwe rahisi. Katika kifungu namba 3(l), mwenye kuleta malalamiko haruhusiwi kuweka barua, viapo ama stakabadhi zingine kwenye hiyo Petition . Hii pia itatatiza wananchi. Wananchi wanafaa kuruhusiwa kuweka stakabadhi zozote ambazo wanaona kwamba zitasaidia kurahisisha kueleweka kwa malalamiko yao na pia kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa sababu wanaleta malalamiko na dukuduku yao katika bunge la kaunti. Lazima hiki kifungu namba (l) kiweze kubadilishwa ili mwananchi aambatanishe stakabadhi zozote ambazo anataka kuleta katika bunge la kaunti ili matatizo yake yaweze kutatuliwa. Jukumu walilopewa karani wa kaunti kuamua kama malalamiko yana ambatana na sheria ama la, ni jukumu kubwa sana. Ninaona kwamba jukumu lile liondelewe kwa karani wa kaunti na liletwe kwa bunge la kaunti. Malalamiko ikipelekwa kwa karani wa kaunti, jukumu lake ni kuyapokea na kuyawasilisha kwa spika naye spika, atawasilisha hayo malalamiko kwa bunge la kaunti. Hilo bunge la kaunti ndilo litaamua kamati ambazo zitashughulikiwa malalamiko hayo. Kama yatakuwa hayana msingi, basi yatazungumziwa katika ile kamati na kuweza kutupiliwa mbali kulingana na vile ambavyo ameomba kufanya. Ningependa kuunga mkono Mswada huu kwa sababu umekuja kwa wakati mzuri. Hii ni njia moja ya kuweza kukuza ugatuzi katika jamhuri yetu ya Kenya. Kumekuwa na usiri mwingi katika uendeshaji taratibu za mabunge ya kaunti na hata hapa katika Senate, ilibidi twende Eldoret ndiposa wananchi waweze kuona jinsi tunavyoendesha vikao vyetu na pia wajue jinsi wanasaidika na Bunge la Seneti. Mabunge ya kaunti yakipewa fursa kama hii ya kutatua matatizo ya wananchi, itakuwa ni rahisi kwa wananchi kupata suluhisho kwa matatizo yao. Pia, itaonyesha kwamba wananchi wanafanyiwa kazi kulingana na vile ambavyo sheria inapendekeza."
}