GET /api/v0.1/hansard/entries/834024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 834024,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834024/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja ya ukosefu wa ajira kama janga la kitaifa. Ningependa kuzungumzia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. Jambo la kwanza, ukosefu wa ajira umefanya vijana wetu kupotea. Wengine wamejiunga na vikundi kama Al Shabaab, na wengine wamekuwa majambazi hapa nchini kwa sababu ya kukosa ajira. Hili si jambo nzuri kwa taifa hili. Ni aibu kubwa sana. Ningependa kuongezea kwa kusema kuwa ukosefu wa ajira hapa nchini unachangiwa na mambo mengi sana. Mambo mengine ni kama vile vikwazo wakati mtu anapotafuta ajira. Wakati kazi zinatangazwa, vijana hawa huwa wamewekewa vikwazo vingi. Kwa mfano, wanatarajia wawe na tajirba ya miaka kumi ndio waweze kuajiriwa. Watakuaje na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}