GET /api/v0.1/hansard/entries/834025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 834025,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834025/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "tajriba wakati hawajawahi kufanya kazi mahali popote? Inamaanisha tunawafungia hawa vijana nje ili wasipate ajira. Watakuaje na tajirba wakati wametiliwa vikwazo vya kuwa ni lazima wawe na stakabadhi za kuwawezesha kuajiriwa? Hawana kazi na wanatakikana kupitishwa na HELB na EACC ilhali hawana pesa. Vijana wengine wanatoka kwa jamii maskini sana ambao hawawezi kuwa na pesa kidogo za kujitetea. Wale wanaotoka katika sehemu za mipakani kwa kimombo tunaziita border districts, wanapata vikwazo kwa sababu wanasoma kwa hali ya shida. Hata wanapofanya mitihani, matokeo yao si mazuri."
}