GET /api/v0.1/hansard/entries/834133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 834133,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834133/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "yangu. Kwa hakika, vijana wengi wameathirika sana na mihadarati. Mambo ya mihadarati imewafanya vijana kuingia katika magenge haramu na hata magenge ya ugaidi. Sisi, kama Wakenya na viongozi, tumefanya machache kuhakikisha tumeweza kuunasua umma wetu na vijana hao wadogo. Kabla hatujazungumzia mambo ya kuwanasua vijana hao ama kuwabadilisha tabia, tujiulize katika taifa letu iwapo taasisi ambazo zinaweza kubadilisha watoto wetu tabia ni ngapi. Pale ambapo kuna taasisi, unapata hakuna walimu, hakuna washauri na pia hakuna vifaa. Utapata ya kwamba pia ni taasisi ambayo mipangilio yake imechanganya watoto wa kike na watoto wa kiume. Hivyo basi kuwafanya watoto wa kike kuathirika na mambo ya ubakaji. Ningependa kuunga mkono sheria ambazo zinasema watoto wadogo ambao wako chini ya miaka 18 wasiwekwe rumande ama jela pamoja na watu wazima. Mara nyingi wanapowekwa katika sehemu kama hizi, badala ya kubadilika tabia, wanaendelea kuwa sugu. Kwanza wale watoto wadogo waliopelekwa jela, wale wazee ambao wamekuwa jela kwa miaka mingi, huweza kuwatumia kwa njia mbaya kama kuwalawiti. Tumepata kesi nyingi sana ambazo watoto wadogo ambao wamepelekwa jela wameweza kulawitiwa hivyo basi kuhatarisha maisha yao. Nataka tujiulize kama Wakenya, sasa hivi, mahakama zetu zimejaa kesi nyingi sana. Kuna kesi za watoto wadogo ambazo bado ziko katika mahakama zetu. Vile vile, tunapata jela zimejaa watoto wadogo na jela zimekuwa na msongamano mkubwa sana mpaka imekuwa hatari kubwa kwa wakenya wengi ambao wanawekwa katika jela hizo. Hii ni njia moja ya kuhakikisha ya kwamba, katika kupunguza kesi ambazo ni ndogo ndogo za vijana wadogo na pia kupunguza vijana wadogo kuwa katika jela na kupunguza msongamano, lazima tuongeze taasisi zinazofaa katika kunasua vijana wetu. Vijana wengi wanaoingia katika mambo kama haya, wengine ni kwa sababu pengine familia zao zimevunjika. Baba na mama wamekuwa mbalimbali na wamewacha majukumu yao juu ya watoto. Wengine pia ni wazazi ambao wamekufa. Kuna majanga ya ukimwi, wazazi ambao wamefariki, mtoto amebaki akirandaranda, hana wa kumuangalia ndiposa anaingilia mihadarati na magenge kama hayo. Je, swala la ushauri, tunalifanya kwa njia inayofaa ama tunalifanya tu ili tuambiwe kwamba tumefanya? Tukiangalia hata katika shule zetu, walimu wa ushauri ni wachache. Utapata shule nzima ina mwalimu mmoja wa Kiswahili na shule hiyo ina watoto zaidi ya mia tano. Je, mwalimu huyu mmoja atamshauri nani amuache nani? Lazima swala la ushauri na walimu wa ushauri wawe wa kutosha ndiposa matukio kama haya ya watoto kuchoma shule yaishe. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}