GET /api/v0.1/hansard/entries/834134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 834134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834134/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Vile vile, lazima walimu waweze kubadilisha riwaya. Kwa kimombo tunasema: “An alternative narrative.” Riwaya ya kwamba mtoto ambaye ni mtundu anakuwa ni adui wa mwalimu ama anatengwa anawekwa kando. Riwaya kama hizi hazitasaidia watoto kama hao. Lazima walimu wawafanye marafiki wale watoto watundu ama wale wameingilia mihadarati, wawaweke karibu, wawapatie ushauri ndiposa tutapata ya kwamba hatutakuwa na watoto wahalifu kama hao. Ningependa kuzungumzia jela na rumande zetu. Tunazijua zilizovyo. Hivi karibuni, katika eneo bunge langu, nilikosana sana na OCS wa eneo la kwangu wakati msichana wa miaka kumi na miwili alikuwa ameshikwa, akawekwa rumande ambako kuna wazee na wanaume chumbani. Msichana wa miaka kumi na miwili amewekwa katika chumba kama hicho! Jamani…"
}