GET /api/v0.1/hansard/entries/834136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 834136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834136/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Ndio nasema tusiwaweke watoto kama hao wa kike katika rumande na kina baba, watu wazima ambao wako pale. Tunajua hisia ni tofauti na wakati jinsia mbili zimekutana mahali kama pale ambapo huwa pana giza, mambo mengi hutokea. Je, hao watoto wetu wa kiume tutawachunga vipi kuhusiana na mihadarati? Katika jela zetu na rumande zetu, kuna wafungwa sugu ambao wanakuwa vichuuzi wa mihadarati, na vijana wanapokuwa pale, mbali na kuwacha mihadarati, wanazidi kuitumia. Unapata sigara zinauzwa na kutiwa mihadarati na maafisa kadhaa kuhusika kabisa kufikisha vitu kama vile katika jela hizo. Lazima tuangalie upeo mkubwa sana, tupige msasa na tujue tutawanasua na kuwasaidi vipi vijana ambao ni zaidi ya asilimia 70. Bila ya kufanya hivyo kuanzia chekechea hadi shule zetu za upili na katika vyuo vikuu, basi jamii hii ya taifa la Kenya itaangamia na hatutaweza kuwa na vijana ambao wataweza kusimamia taifa letu na kuendeleza maendeleo. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii."
}