GET /api/v0.1/hansard/entries/834445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 834445,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/834445/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ruiru, JP",
"speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
"speaker": {
"id": 13468,
"legal_name": "Simon Nganga Kingara",
"slug": "simon-nganga-kingara-2"
},
"content": " Asante sana, Bwana Spika kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Niko katika Kamati ya Ardhi and ni vizuri niunge mkono Hoja hii kwa sababu ina uzito kimaendeleo. Kama vile wananchi wanajua, chochote kinachotendeka katika nchi yetu huwa kinahusiana na ardhi. Ardhi ni muhimu. Hoja iliyo mbele yetu inahusu ardhi na umaskini. Ardhi ndio huleta umaskini au utajiri. Kama vile imechangiwa hapa, duniani, utaratibu na upangaji wa ardhi uko wa hali ya juu sana. Wakenya wanastahili kusoma Ripoti hii. Tumeiangalia vizuri na tukaona kuna uzembe kidogo. Hata katika yale maeneo yaliyo karibu sana na Jiji la Nairobi, cheti na utaratibu wa upangaji wa ardhi bado uko nyuma kidogo. Kama vile Ripoti imeonyesha, yale maeneo ambayo yameendelea, haswa maeneo ya Ulaya, unapata kuwa kama eneo limetengwa kuwa la kilimo, linakuwa la kilimo. Kama eneo limetengwa la viwanda, linakuwa la viwanda. Huo ndio utaratibu tunaopaswa kuiga kama Wakenya ili tuone kama nchi yetu itaendelea. Kuna changamoto kubwa sana. Wakati una shamba na huna cheti, huwezi kujenga nyumba ya kudumu kwa sababu hujui kesho itakuwa vipi. Ni jambo la busara kwetu sisi kuchukua hatua kutumia teknolojia kupata cheti au mpango mwafaka wa ardhi ili watu waweze kufanya kazi ya kufaa katika mashamba yao. Uzembe mwingine ulio katika nchi yetu - na nimejaribu kuleta Mswada kuhusu jambo hili - ni maeneo yaliyotengewa mambo maalum, haswa shule na hospitali. Maeneo haya hayana vyeti na yanatumika kiholela. Ndio maana Mbunge mwenzangu akasema kuwa wakati Serikali inataka kuendeleza miradi, inakuta lile shamba lilinyakuliwa na inaigharimu Serikali pesa nyingi sana kurudisha lile shamba mikononi mwake. Kwa hivyo, tukitumia hii Ripoti kama kielelezo cha kutumia ardhi kupunguza umasikini na haswa kuendeleza nchi, Kenya itakomaa na kuendelea kama nchi zingine duniani. Ni jambo la kuhoofisha sana ukiangalia yale maeneo yametuzingira. Hawana shida ya ardhi kama Kenya. Ingawa Kenya inajaribu, bado tuko nyuma. Kuna swali umeuliza hapa. Tumesoma Ripoti hii, lakini, sasa tutafanya nini? Ni jukumu letu sisi Wanakamati na Wabunge The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}