GET /api/v0.1/hansard/entries/835019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835019/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Wale watu waliokuwa wakiishi katika Kijiji cha Marmanet, hasa pale katika msitu, walifukuzwa mwaka wa 1988, na wanaishi katika hali ya ufukara mkubwa sana. Tukiangalia katika sehemu zingine, watu waliofukuzwa katika sehemu za misitu walipewa makao mengine mbadala. Kwa mfano, wale waliofurushwa kutoka katika Msitu wa Mlima Kenya walipewa makao mahali panapoitwa Solio. Lakini ukitembea huko Marmanet, kuna zaidi ya watu 10,000 wanaoishi katika hali ya ufukara mkubwa. Wanaishi katika vijiji ambavyo havina mashule au maji; wanaishi katika hali mbaya sana. Ningetaka kuuliza Kamati ya Seneti itakayopewa jukumu hili – hasa ile inayohusika na mambo ya mashamba – watembee pale kwa sababu watakapoona ile hali ndugu na wazazi wetu wanayoishi pale, watajua kwamba wanaishi kana kwamba hawako katika nchi hii ya Kenya. Hii ni kwa sababu umaskini umekithiri pale, ilhali wao ni Wakenya. Tulipokuwa tukiandika hii Petition ili tuilete hapa, tulishangaa kwamba wale watu wamekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu sana. Wamekuwa wakiambia Serikali zilizokuwa nyakati hizo, lakini hawakuchukuliwa kama Wakenya, na hawakupewa umuhimu unaofaa. Kwa hivyo, tunaiomba ile Kamati itakayopewa jukumu hili ifuatilie ili tujue ni kwa nini watu hao wa Laikipia wanachukuliwa kama wao sio wananchi wa Kenya hii. Hali yao ni duni, hawana mashamba, nyumba, shule wala hospitali. Wanaishi katika hali ya ufukara."
}