GET /api/v0.1/hansard/entries/835178/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835178,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835178/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, cha kusikitisha kabisa ni wakati magaidi waliposhambulia Chuo Kikuu cha Garissa ambako wanafunzi wengi walipoteza maisha yao bila ya hatia yoyote. Kwa hivyo, ugaidi umekuwa ni janga la Taifa na umesababishwa zaidi na mafunzo ya itikadi kali ambayo yanafanywa na wale wanaoongoza vikundi vya kigaidi ambavyo vimeingia katika jamii yetu, na imekuwa vigumu kwa asasi za kitaifa kama vile polisi wahaohusika na anti-terrorism kuwatambua watu kama hawa na kuwatoa, ili vijana wetu wasiweze kujiunga na vikundi hivi vya itikadi kali za kidini. Bw. Spika wa Muda, nikizungumzia sehemu ya Mombasa na pwani kwa jumla, vijana wengi sana wametoweka na kwenda sehemu ambazo, wengi wanatumiwa na wanaojifunza mafunzo ya kigaidi. Kwa mfano, wengi walikwenda Somalia na kujiunga na kundi la Al Shabaab, na wengine wakaenda hadi Syria ili kupigana na mambo ya jihadi ambayo ni kinyume na dini ya Kiislamu. Bw. Spika Wa Muda, sheria zilizoko kwa sasa zinaupungufu. Hii ni kwa sababu wengi walioenda katika safari za kigaidi wakirudi, jamii inawakataa. Wanapokataliwa na jamii, hawajui iwapo waende kwa polisi au wajifiche. Hii ni kwa sababu wakienda kwa polisi, tayari wana hatia, na wakijificha, polisi watawasaka na kuwaua bila hatia yoyote. Vilevile, hawawezi kurudi kule walikotoka kwa sababu watachukuliwa kama wasaliti kisha wauawe. Kuna vijana wengi hasa kutoka sehemu za Kwale na Mombasa ambao walirudi kutoka Somalia na wakapoteza maisha yao kwa hali kama hizo."
}