GET /api/v0.1/hansard/entries/835179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835179,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835179/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Serikali imewapoteza vijana wasiopungua 300 sehemu ya Mombasa na kwingineko Pwani kwa sababu ya tuhuma kwamba wanashirikiana na magaidi. Mmoja katika vijana hawa ni Bw. Husni ambaye alichukuliwa mwezi wa tano mwaka huu na hadi sasa hajulikani alipo. Ijapokuwa sheria iliyoko sasa inalinda wananchi na mambo ya ugaidi, ina upungufu fulani ambao lazima ufanyiwe marekebisho ili iweze kusaidia."
}