GET /api/v0.1/hansard/entries/835186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835186,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835186/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, jambo lingine nzuri ambalo limekuja na Mswada huu ni kwamba kunatakiwa kubuniwa taasisi za kurekebisha tabia za wale waliosafiri kwa maswala ya itikadi kali na pia ugaidi. Kuna wakati ambapo wengi waliorudi walikuwa wakipelekwa Matuga Technical Training College, lakini baada ya kutoka kule, wengi wao waliachwa kivyao bila makaazi. Wale magaidi walioandamana nao safarini kule Somalia au kwingineko, wanarudi kuwaua kwa sababu wanachukuliwa kama wasaliti. Kwa hivyo, tukipata taasisi za kurekebisha tabia, wengi watapata mafunzo ili waweze kutumikia maisha yao kwa njia ya amani na kusaidia jamii katika mambo tofauti."
}