GET /api/v0.1/hansard/entries/835188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835188,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835188/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ninaunga mkono Mswada huu wa kurekebisha hii sheria ya ugaidi ili iwasaidie waathiriwa wa itikadi kali na vilevile wale waliofungwa kwa sababu ya ugaidi. Pia twaomba Serikali iangalie sana maswala ya vijana wanaopotea hivi sasa. Hii ni kwa sababu wengi wanapotea kwa mikono ya polisi ama taasisi za Serikali zinazolinda usalama wa nchi. Kwa sasa, kama nilivyotangulia kusema, kuna vijana zaidi ya 300 waliochukuliwa. Tulileta Hoja hiyo hapa na kutoa Statement, lakini hadi sasa hatujaona marekebisho yoyote ama dalili zozote kwamba hawa vijana wataachiliwa."
}