GET /api/v0.1/hansard/entries/835219/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835219,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835219/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ahsante, Bi. Spika wa muda, kwa kutamka jina yangu sawa sawa. Ahsante pia kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mswada huu ambao unataka kufanya mageuzi kwa sharia dhidi ya ugaidi na kuifanya iwe mwaafaka. Ningependa pia kumuunga mkono na kumpa hongera Bi. Seneta mteule, Sen. (Rev.) Waqo. Inasemekana ya kwamba Wako nyingi ni yale ambayo yako na konsonanti ‘k’ lakini nilipokuja Seneti mara ya pili, nilipata kujua ya kwamba kuna Waqo ambayo iko na konsonanti ‘q’. Amefanya juhudi na ninampa hongera kwa kuleta Mswada huu ili tuipige pasi hii sharia na kuifanyia mageuzi ili iweze kufaa jamii ya wakenya. Sio jambo jipya kuona ya kwamba watu wetu wanaingia katika vikundi vya ujangili kwa urahisi ili kuletea binadamu shida. Tunajua ya kwamba ujangili ama ugaidi haiko Kenya peke yake bali iko ulimwengu mzima. Tunafa kuweka mkazo hapa nyumbani kwa sababu tumeona vijana wetu wengi wakijiunga na vikundi vya ugaidi kwa urahisi sana. Haya yote yanaletwa na ukosefu wa kazi na utendaji wa shughuli fulani. Wengi huacha masomo wakifika kiasi fulani. Hata wale ambao wamesoma wakafika katika vyuo vikuu, unapata ya kwamba wale watu wanaweza kuwafikia na kuwatia katika vikundi vyao vya ugaidi. Tumeona ya kwamba imekuwa rahisi vijana wetu kuingizwa katika vikundi hivi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu na serikali imeweza kuchangia hali hii. Jamii ya Kenya na serikali yetu inafaa izingatie jinsi ya kuwalinda wananchi wake, haswa vijana ambao ni wa kike na wakiume. Hii ni kwa sababu katika ugaidi, tumeona wavulana na wasichana wetu, wakiwa watoto ama watu wazima, wakihusishwa katika mambo haya na wameingia katika vikundi vinavyofanya mambo ya ujangili. Serikali yetu inatakikana kujenga polytechnics ama shule ya kufundisha mtu anapomaliza shule kwa sababu hawa vijana wanahitaji kupata vibarua. Polytechnic imekuwa ghali na hawa vijana wamekuwa wananchi ambao hawafanyi kazi. Kina mama wetu ambao hawafanyi kazi wanategemea kulima vipande katika shamba ya watu wengine ili wapate chakula ya kukula na kulisha watoto. Imewabidi kuwapeleka watoto wao katika polytechnic kule vijijini na hiyo hali ni duni. Ikiwa tutapitisha hii Mswada, serikali itatakikana iende chini kuhakikisha ya kwamba watoto wetu wameepuka mambo kama haya. Tukitaka kupigana na jambo hii, inafaa ya kwamba watoto waweze kwenda katika polytechnic wakimaliza shule ili wajifundishe kitu fulani ambapo wakimaliza, watakuwa na shughuli ya kufanya na hii inaweza kuwa useremala ama kutengeneza baiskeli. Katika huu Mswada, nimeona kipengele cha 12(e) ambapo kuna mikakati ambayo tunaweza fanya ili hawa watoto waweze kuelimishwa na kupata kazi ya kufanya. Ningependelea ya kwamba tuweke mkazo ili watoto wakimaliza shule waweze kupata kazi ya kufanya. Isiwe ya kwamba mtu anamaliza kidato cha nne na hana pakuenda. Akiangalia polytechnic, anapata ya kwamba imekuwa ghali na mama yake amebaki nyumbani na hawezi kumusaidia na chochote. Mzee pia hawawezi kumusaidia kwa sababu hana kazi na wala hana ndugu mwenye anafanya kazi. Kwa hivyo, anakuwa mtu amesoma, amefika kidato cha nne, darasa la saba ama chuo kikuu lakini hana kazi. Itakuwa rahisi sana shetani afanye kazi kwa akili ya mtu kama huyo na ndio wazungu wakasema ya kwamba; it is a devil’s workshop . Yaani, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}