GET /api/v0.1/hansard/entries/835220/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835220,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835220/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "shetani atafanya kazi yake anayoijua katika akili ya yule kijana ama yule dada. Kwa hivyo, kipengele kama hiki ni muhimu na ninaiunga mkono ili tuweze kufanya mageuzi ndiposa ipatikane katika sheria zetu za kupambana na mambo ya ugaidi. Jambo lingine ningependa kuzungumzia ni vijana kupigwa risasi na kuuawa katika mkoa wa Pwani; Mombasa, Kilifi na Kwale. Sio wengine wanaofanya jambo kama hili ila ni polisi. Jambo hili linafanywa na watu ambao wanasilaha. Mara nyingi ukienda kuuliza baada ya siku mbili au tatu kuhusu mtu ambaye amepigwa risasi, utaambiwa ya kwamba ‘hatujui ni nani alimuua’. Visa kama hivi vinafanya watu wawe na ugumu kukubaliana na yale mambo ambayo wanaambiwa kuwacha. Badala yake, hao husema ‘waliuwa baba yangu, waliuwa ndugu yangu au shangazi yangu na mimi pia nitalipiza’. Kwa hivyo, kunatakikana kuwe na elimu au hoja kama hii. Tunafaa kuiunga mkono kwa sababu tunatafuta jinsi tunavyoweza kusaidia wakenya kwa sababu ukiangalia ugaidi siku hizi, utapata kuwa kuna mjaluo, mluhya, mkalenjin, mturkana, mgiriama, mmijikenda na hata mswahili kama kuna kitu kinaitwa Swahili. Ninasema hivyo kwa sababu sisi huwa tunawaita waswahili wajomba kwa sababu walikuwa watoto wa aunties . Kila jamii ya Kenya ama kabila iko ndani ya Al-Shabab, Mombasa Republican Council (MRC), Chinkororo, Jeshi la Msambwa, Jeshi la Mzee ama Sabaot Land Defence Force (SLDF) ya Mt. Elgon."
}