GET /api/v0.1/hansard/entries/835221/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835221,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835221/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Magenge kama haya yanafaa kuangaziwa ili tumalize ugaidi. Wakati Serikali inatafuta bunduki zilizopotea, wanafaa kupeana amnesty kwa walio na bunduki bandia wazirejeshe ili wasamehewe. Watu wengi wanajiunga na vikundi vya ugaidi. Wengi wako hapa Kenya na wengine wako Somalia. Ndio maana wanajeshi wa Kenya Defence Forces (KDF) wako kule Somalia kwa sababu sote hapa tunataka amani ambayo haiwezi kuwepo bila sisi kuwa na majeshi yetu Somalia. Hata hivyo, hiyo sio suluhu pekee. Tunafaa kuzingatia kuwa kuna watoto wetu kule na ikiwa wataondoka--- Kwa mfano, kuna mmoja aliyekuwa akilia kuwa hana miguu na mikono kutokana na pengine kulipuliwa kwa bomu au kukatwa na watu kwa sababu hakushirikiana nao. Lazima Serikali ipeane amnesty kwa watoto wetu waliojiunga na kundi la Al-Shabaab ama magenge mengine kama vile Chinkororo, Mombasa Republican Council (MRC), Jeshi la Mzee na kadhalika na hatimaye wakajiondoa. Kuwe na amnesty kwa mtu yeyote aliyekosa na kuomba msamaha baada ya kuachana na mambo ya terrorism ama ujangili. Anafaa kupewa nafasi kuwa mmoja wa Wakenya “waliojisafisha” kama vile Wakristo husema kuwa wameokoka na hawatafanya dhambi tena. Lazima tuangalie jinsi ya kuwachunguza wakijitokeza kwa nia safi. Wanafaa kuangaliwa tabia mikononi mwa Serikali bila kuadhibiwa. Wanafaa kukubaliwa na jamii na hata kupewa ajira wakati kuna nafasi za kazi."
}