GET /api/v0.1/hansard/entries/835222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835222,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835222/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tuko hapa sote kama Wakenya. Ikiwa nchi hii itaharibika, Wakenya wa tabaka zote wataharibikiwa. Hatuwezi kusema kuwa ugaidi unafanywa na Waislamu ama Wakristo. Vile vile, hatuwezi kusema kuwa unafanywa na watu ambao hawana dini. Ugaidi unahusu kila mtu; awe Mkristo au Mwislamu. Tumeona vijana wetu wa dini za Kikristo na Kiislamu na vile vile wasiokuwa na dini wakijiunga na ugaidi. Tumeshuhudia vijana wetu wa tabaka mbalimbali za Kenya wakijiunga na makundi ya kigaidi niliyotaja hapo awali. Kwa hivyo, Serikali inafaa kuhakikisha kuwa Kifungu hiki cha 12 kinawekwa mwafaka. Baada yao kupewa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}