GET /api/v0.1/hansard/entries/835229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835229/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Seneta aliyezungumza kabla yangu, Sen. Madzayo, alisema kuwa ugaidi hasa unaletwa na ukosefu wa ajira na ni kweli. Vijana ambao hukosa ajira na kubaki nyumbani hukosa jambo la kufanya na kuingilia ulevi. Hatimaye wanaingia katika ugaidi kwa sababu wale wanaouendeleza huwaambia watawalipa vizuri. Kwa hivyo, ni jukumu la serikali za kaunti na Serikali ya kitaifa kupatia vijana wetu majukumu. Wale waliosoma wanafaa kupata vibarua ili wasijiingize katika ugaidi. Bi. Spika wa Muda, ugaidi unarudisha nyuma jamii iliyostaarabika na ambayo inataka kuendelea. Kuna mambo ambayo hufanyika kule Pwani ambayo ni ya kuvunja moyo sana. Wakati wa kushambulia magaidi, tumeona jamii fulani ikiathirika sana katika vita hivi. Misikiti ya Waislamu mjini Mombasa imevamiwa na askari. Vile vile Waislamu kwa jumla wamehusishwa na ugaidi ilhali tunajua kwamba ugaidi hauambatani na dini kwa njia yoyote. Tumewaona polisi wakivamia misikiti kule Mombasa na kuleta vurugu. Hali hiyo haiwezi kukomesha ugaidi kwa sababu magaidi hawako katika dini yoyote. Ni watu waliotoka katika dini na wamelaaniwa kwa sababu huwezi kuua watu kisha ujiite Muislamu. Ukifanya hivyo utakuwa unaharibu jina nzuri la Kiislamu kwa sababu Quran inasema kwamba mwenye kutoa roho ni Mungu pekee wala sio kazi yako. Anayejiingiza katika hali ile anawaharibia jina watu wa dini hiyo."
}