GET /api/v0.1/hansard/entries/835271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835271,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835271/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, tulikuwa hapa mwaka wa 2013 katika Bunge la Kumi na Moja. Wakati huo hatukuwa na sheria ambapo wananchi wangepewa nafasi ya kutoa malalamiko yao katika Bunge. Nina furaha kuwa sheria zetu zinawezesha watu wetu katika kaunti zetu au mtu binafsi kuleta malalamiko yake mbele ya Seneti hii na kusikilizwa. Jambo hili lilikuwa limeleta joto nyingi kwa MCAs wetu katika Serikali za Ugatuzi kutosikizana. Na tulikuwa na hiyo shida katika Bunge la Kumi na Moja. Lakini hivi sasa nimeona ya kwamba mmezingatia huu Mswada ambao umeletwa na dada Sen. Pareno. Nimeona ya kwamba hii sheria ambayo itatusaidia katika hizi harakati zetu, za kuweza kusikiza malalamiko kutoka kwa wananchi, kaunti zetu sote na taifa kwa ujumla. Nimetafakari zaidi sana juu ya Mswada huu. La umuhimu zaidi ni kwamba tulikuwa na maombi tuliyoipata katika Bunge la Kumi na Moja ikiwemo malalamiko makubwa kutoka kwa Gavana Mwangi wa Iria wa Kaunti ya Murang’a na Gavana wa Kaunti ya Embu. Na kwa sababu ya upunguvu wa sheria fulani waliweza kutumia vipengele fulani vya Katiba na wakaweza kufaulu. Seneti ikawa haina mamlaka yoyote isipokuwa kuangalia tu na kutii uamuzi wa korti. Hawa watu wakaendelea kuwa ofisi japokuwa Seneti ilipitisha sheria ya kuwaachisha kazi. Lakini haikuwezekana kwa sababu ilibidi waende katika Mahakama Kuu na wakaweze kuzuia mapendekezo ya sheria zile ambazo zilikuwa na upungufu, hasa kuweza kukumbaliana na pendekezo ama lalamiko la wananchi au la mtu binafsi kutoka mashinani. Mwanzo sheria hii ambayo tumeiweka ama tunataka kuiweka ama iko katika zile harakati za kuiweka ni sheria ambayo itaweza kuweka mwangaza, na kuleta njia mwafaka yakwamba ikiwa kuna mtu anahitajikuleta malalamishi yake katika serikali za mashinani, basi iko njia anayoweza kufuata kama mwananchi na halafu atapewa fursa ile yeye kuja na kuweza kuitetea ile. Nimeona tunaweza kuweka lalamiko hili kwa lugha ya Kiswahili ama Kiingereza. Maoni yangu ni tupee kipao mbele malalamiko kama haya yanayotoka mashinani. Tunajua wote walioko huko mashinani wanaelewa na kusikia lugha ya Kiswahili. Nikimwambia nyanyangu aandike Petition au lalamiko lake katika lugha ya Kiingereza itakuwa vigumu kwake kufanya hivyo. Ni maoni yangu kuwa serikali za mashinani na mabunge yao, yatilie mkazo matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli zao za kila siku ili wananchi wetu wafaidike sana. Kipengele cha 4(4) na (5) cha Mswada huu kinasema kwamba malalamiko yoyote hayawezi kutupiliwa mbali na katibu wa bunge la kaunti. Mara nyingi kumekuwa na upungufu wa watu kutoelewa aidha katika malalamiko hayo ama katibu yule asipolielewa vizuri anaweza kutumia sheria vibaya na kusema kwamba “ombi hili halikuandikwa vizuri, kwa hivyo sitaikubali.” Makatibu sasa wanamulikwa na hawawezi kukataza malalamiko kwa sababu hayakuletwa kiusawa au kisheria bora tu yawe ni malalamiko. Hatutaki kumpatia katibu wa bunge la kaunti mamlaka ambayo baada kuangalia ombi la wananchi anaamua halikubaliki kwa sababu ni kinyume cha sharia na kumsihi spika kulitupilia mbali. Ikiwa malalamiko hayo yametumwa kwa bunge la kaunti kupitia kwa spika au katibu wa bunge The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}