GET /api/v0.1/hansard/entries/835272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835272,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835272/?format=api",
"text_counter": 352,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "la kaunti, ombi hilo litakubaliwa. Kipengele kama hiki kinazuia utumiaji vibaya wa mamlaka katika serikali za kaunti. Tumegundua kwamba wakati mwingi, sheria zinatumiwa vibaya, haswa katika serikali za kaunti. Sheria hii itaweza kuweka mwelekeo ama mwangaza kisawasawa kisheria ili kila mtu ambaye ana jukumu kama katibu asitumie sheria hii kukataza malalamiko ambayo yamewasilishwa na mwananchi kwa bunge la kaunti ama serikali ya kaunti kwa misingi kwamba haikuzingatia muundo wa kuwasilisha ombi hilo kwa bunge. Tunataka kupitisha sheria hii ili itumike vivyo hivyo. Pia, maagizo ya vile watu wanaweza kuja pamoja na kuongea juu ya malalamiko yao, sheria hii itakuwa nzuri kwa sababu mara nyingi watu wanakatazwa nafasi za kuongea, haswa katika mashinani, wakati wowote ikiwa wana malalamiko. Kwa hivyo, sheria hii ambayo tunataka kupitisha itasaidia serikali za kaunti kutatua malalamishi ya wananchi yanapokuja ni kwamba wao wasiwe na uwezo wa kuzuia mtu yeyote kuwasilisha malalamiko yake kwetu au kwa bunge la kaunti na hatimaye bunge hilo la kaunti kuwasilisha malalamiko hayo kwa Bunge la Seneti. Sisi tukiwa kama baba yao, ama waangalizi maalum kama Bunge la Senate ambalo linaangalia maslahi ya serikali za kaunti. Naunga mkono zaidi na kumpatia hongera Sen. Pareno ambaye sisi sote ni kama wahamiaji - tunahama hama hapa na pale lakini hayo ni baadhi ya mambo mengine tukitafakari. Nataka kuunga mkono sheria hii ambayo inaweza kuangalia majukumu ya"
}