GET /api/v0.1/hansard/entries/835996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 835996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835996/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, natuma risala za rambi rambi zangu na watu wa Kaunti ya Laikipia kwa familia za wale walipatwa na mkasa huu. Ni jambo la kuhuzunisha sana kwa sababu imekuwa ni kama jambo la mazoea kwetu hasa kama nchi kuwa hatupei umuhimu mambo ya watu ambao wana husika katika ajali. Ajali hutendeka, na mambo yana endlea. Swali ambalo tunafa kujiuliza ni kwamba: Wakati tulikuwa na Waziri Michuki sheria ilifuatwa zaidi kama vile tuko na Waziri Matiangi. Unapata ya kwamba ikiwa Waziri fulani ako katika Wizara fulani, sheria zina fuatwa. Ningependa kusisitiza kwamba sheria zinafaa ziandikwe katika nyoyo zetu kama Wakenya. Kila wakati ukipita barabarani kuna Askari. Lakini wakati mwingine magari mengine yana beba zaidi ya kiwango chao. Kama vile tume ambiwa, lile gari lilikuwa limebeba kushinda kile kiwango kimewekwa. Kutoka Nairobi hadi zile sehemu, kuna askari ambao wana simama katika hizo barabara. Inaonekana hawa watu wamezembea katika kazi zao. Tukichukulia mwenye gari hatua, tunapaswa pia tuwachukulie hatua polisi hatua, hasa wale waliokuwa katika zile sehemu za barabara ambako lilegari lilipitia. Walikuwa wakifanya kazi gani ikiwa kazi si kuangalia vile lile gari limebeba? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}