GET /api/v0.1/hansard/entries/835999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 835999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/835999/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, kuna matamshi ya kusema ya kwamba yule dereva alikuwa zaidi ya miaka sabini. Sitaki kusema mtu wa miaka sabini hawezi kuendesha gari. Lakini yule ni mtu ambaye ni rahisi sana kuchoka. Kwa sababu ya huo umri tunakubali ya kwamba itakuwa si vizuri aendeshe gari. Kama nchi, tunafa tupitishe sheria. Hata sheria ya Kenya inasema kwamba mtu akifika miaka 60 anapaswa kustaafu. Huyu alikuwa katika kazi ya uma, ana endesha watu wengi. Akiwa na ile miaka hapaswi kuendesha gari ya uma. Bw. Spika wa Muda, nasisitiza kwamba Waziri anayehusika anafaa afanye kazi yake. Pia tunafa tujitole na sheria ziwe zimeandikwa katika mioyo yetu. Si kuacha watu waingie katika gari ambalo tayari limejaa; wengine wana zidi kuingia. Ni vizuri kama watunga sheria tutuengeneze sheria. Waziri Michuki hakutunga sheria mpya. Sheria ziko, shida ni watu kutozifuata. Askari ambao wanapaswa kufuatilia sheria wanapaswa kufanya kazi yao. Katika sehemu zingine duniani, ajali kama hii ikitendeka, Waziri hujiuzulu kwa sababu anapaswa kuchukua hilo jukumu kusema kuwa: “Kama Waziri anaye shughulikia na mambo ya barabara, nafaa kutumikia Wakenya.” Mkuu wa Polisi anapaswa kuwa amewacha kazi kwa sababu imeonekana wazi wale wanao zembea katika kazi yao. Bw. Spika wa Muda, nachukua nafasi hii kutuma risala zangu za rambi rambi kwa jamaa na marafiki. Tunatakia familia hizo heri njema. Mwisho, ya Mungu hayawezi yakafanyika chochote. Asante kwa kunipa fursa hii."
}