GET /api/v0.1/hansard/entries/836004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 836004,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836004/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nitume risala zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki waliopoteza maisha ya wapendwa wao katika ajali hii ya barabarani. Bw. Spika wa muda, ajali za barabarani zimekuwa kawaida katika maisha ya Wakenya. Sielewi kwa nini askari wa trafiki wapo barabarani. Kwa nini tusiwaondoe askari wote kutoka barabarani hapa Kenya? Tumewaajiri askari hawa barabarani ili kulinda na kuangalia iwapo magari haya yamebeba watu kiwango kinachostahili. Wakati askari hawa wako barabarani na magari yanabeba watu zaidi ya kiwango kinachotakikana, yanaenda kuanguka kila siku na kumaliza watu. Baada ya watu kufa barabarani ndio tunakuja kutuma risala zetu za rambirambi. Ni kweli kwamba aliyefiliwa na watu wake anafaa kupewa risala za rambirambi. Lakini itakuwa haina maana iwapo tutaendelea kutuma risala hizo iwapo magari hayo yataendelea kuua watu katika barabara za Kenya. Wakati umefika tuseme yale The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}