GET /api/v0.1/hansard/entries/836007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 836007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836007/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "yaliyoharibika mbeleni yameharibika, lakini kwa wakati huu, turekebishe hali hii katika barabara. Bw. Spika wa muda, tulikuwa na shida ya askari barabarani kuchukua pesa na kupitisha magari mabaya. Tumeongeza National Transport Safety Authority (NTSA), ambao wako barabarani. Maafisa wa NTSA pamoja na askari hawalindi magari na hawawajibiki katika kazi yao. Tumeendelea kukaa na askari wanaendelea kuchukua pesa; na sio mara moja au mara mbili, bali hayo ndio yamekuwa maisha ya Wakenya. Ni aibu kubwa sana katika nchi hii kwa sababu watu wanaendelea kufa, sheria hazifuatwi na watu wanajazana katika magari mpaka wanasimama. Magari huanguka kila siku kwa sababu kuna mtu amelala na kuzembea kazini. Ni lazima tuseme kwamba wakati huu, tumetosheka na hatuwezi kukaa na kuangalia wananchi wakiishia barabarani. Bw. Spika wa muda, kama vile wenzangu walitangulia kusema, hatari kubwa ya watu kuisha kwa wingi iko katika barabara za Kenya zaidi ya wale wagonjwa walioko hospitali na majumbani. Watu hawajali. Wako wapi wale watu waliopewa majukumu ya kushughulikia barabara zetu? Yuko wapi Waziri wa barabara na usafiri? Kwa nini Marehemu Michuki, alipokuwa akishughulikia barabara, mambo yalikuwa yakiendelea vizuri? Kwa nini saa hii tunalala kazini? Kwa hivyo, Bw. Spika wa muda, ni lazima sote tuwajibike na tuwache mambo ya kutuma risala za rambirambi baada ya watu kuisha. Lazima kila mtu awajibike katika Kenya hii ili tuweze kuishi kama nchi ambayo barabara zake ni salama, na utendakazi pia uwe ni ule ulio sawa kabisa. Bw. Spika wa muda, nachukua nafasi hii hasa kupeleka risala zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao; nawaambia poleni. Asante, Bw. Spika wa muda, kwa kunipa nafasi hii."
}