GET /api/v0.1/hansard/entries/836031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 836031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836031/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwa uhakika wakulima wa mahindi katika nchi hii wanafaa kupewa heshima. Pia inafaa zile changa moto ambazo wanazipitia zichunguzwe. Magala yamejaa mahindi ya misimu iliyo pita. Nazungumza kwa uhakika kwa sababu natoka sehemu ambayo mahindi inakuzwa. Ukisafiri katika barabara za nchi hii, utakuta mahindi inamea kila sehemu hasa katika msimu wa mvua. Mahindi haya yanauzwa kando ya barabara, hayapati soko halisi. Wanaopanda haya mahindi wanataka kutumia wanachopata kugharamia mahitaji ya kinyumbani kama karo na kununua chakula. Mahindi ni chakula halisi ya Waafrika hasa Wakenya. Mahindi huliwa katika nyanja mbali mbali. Wengine huisaga na wengine hutengeneza Githeri. Tunafaa tuchunguze zile changamoto ambazo wakulima wa mahindi hupitia. Hakuna njia tunayoweza kujua hali yao bali inafaa tutumie Kamati hii ili ichunguze na ituletee Ripoti katika Seneti hii ili tuweze kutatua matatizo ya wakulima wa mahindi na swala la mahindi kukosa soko. Kamati hii imenadika na kusema wakati ambao ilipewa hautatosha kuleta habari kamili kuhusu wakulima wa mahindi. Ni kweli tunafaa kuwapatia nafasi ili waweze kutuandikia Ripoti ili tuijadili katika Seneti hii. Pia tunafa tusiwavunje wakulima wa mahindi moyo kwa sababu msimu mwingine wa mvua utaanza hivi karibuni na watu tayari wame jitayarisha kupanda mahindi. Natumaini Kamati itaandika Ripoti hiyo vizuri ili tuweze kutatua matatizo ya wakulima. Tukifanya hivyo, wenye kupanda mahindi watakuwa na moyo na wataweza kuendeleza ukuzaji wa mahindi. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii ili Kamati hii ipewe nafasi zaidi ili watembee nchini na waweke matatizo yote katika Ripoti. Asante kwa kunipa fursa hii."
}