GET /api/v0.1/hansard/entries/836069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 836069,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836069/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi nyingine tena. Nampongeza rafiki yangu, Sen. Olekina, kwa kuleta Hoja hii mbele ya Seneti. Hakika, tunafaa kuukuza utalii ndani ya Kenya. Kuna mambo mengi maridadi yaliyo mafichoni humu Kenya, ambayo tunafaa kuyatoa nje ili kuvutia watu wengi. Kwa hakika, hakuna kaunti ambayo haina mambo mazuri ya kitalii, lakini mengi ya hayo yako mafichoni. Bw. Spika wa Muda, tunafaa tubadilishe mtazamo wetu kuhusu utalii, kwa sababu sisi tunafikiria kwamba watalii ni wale wanaotoka nchi za nje kuja hapa peke yao. Mambo mengi mazuri ya utalii yako ndani yetu, kwa mfano, jinsi Waafrika tofauti wanavyoishi na mambo mengine mengi. Vijana waliozaliwa nyakati hizi za tarakilishi hawafahamu mambo mengi katika kaunti zao. Wengi wao hata wamesahau lugha ya mama. Tukirudi katika kaunti zetu, tutaona mambo mengi ambayo tunaweza kuyaweka nje ili kuwavutia utalii. Kwa sababu hiyo, tunatakikana kugeuza mtazamo wetu kuhusu utalii, ambapo tunafikiria watalii ni Wazungu peke yao wakija katika sehemu hizi ili kuangalia mambo yetu hapa. Lakini hata sisi pia, kama Waafrika, tunaweza kukuza utalii wetu. Bw. Spika wa Muda, ukienda maeneo ya bahari, ambako watu wanapenda kwenda, watalii wengi walio huko kwa wingi sio Wazungu vile tunavyofikiria, bali ni watalii wa hapa nyumbani. Kwa sababu hiyo, tunapasa kuukumbatia, kuukuza na pia kuunga mkono utalii wetu. Hii ndio sababu nimechukua fursa hii ili kuunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}