GET /api/v0.1/hansard/entries/836412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 836412,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836412/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, ODM",
"speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
"speaker": {
"id": 13379,
"legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
"slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
},
"content": "Nataka niseme ya kwamba, mazingira ya nchi yetu yanazidi kuzorota kwa sababu lile shirika ambalo limepatiwa nafasi ya kulinda na kuchunga mazingira ya nchi hii, limelala ama wanazembea. Ukiangalia katika Ripoti ambayo imeletwa hapa leo na Kamati hii ya Mazingira, inaonyesha kwamba Shirika la NEMA lingekuwa limefunga hii kampuni kitambo sana na sio kwa sababu ya hii Ripoti. Kampuni ya LDKL ilipatiwa nafasi ya kufunga na kuhakikisha kwamba imerekebisha ile shida ambayo iko na hawakufanya hivyo. Hii inamaanisha ya kwamba shirika la NEMA limezembea. Tunaona ya kwamba kuna hizi nyumba ambazo zilikuwa zimepatiwa leseni na NEMA zijengwe kwenye mito. Shirika la NEMA ndilo limesababisha mambo kama hayo. Ukienda kule Kibarani, unaona ya kwamba bahari imejazwa na uchafu hivi sasa. Shirika la NEMA linaangalia lakini hawafanyi chochote."
}