GET /api/v0.1/hansard/entries/836414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 836414,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836414/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, ODM",
"speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
"speaker": {
"id": 13379,
"legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
"slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
},
"content": "Pia, ningependa kusema ya kwamba ile kampuni ya LDKL imeonyesha ya kwamba iko na madharau. Waliambiwa wafunge ili warekebishe lakini hawajafanya chochote mpaka sasa. Hii inamaanisha ya kwamba hawajali afya ama mazingira ya nchi hii ya Kenya. Wao wanafikiria mambo ya senti na matumbo yao pekee yake. Kwa hivyo, ni lazima sisi, kama Bunge, tusimame kidete tuhakikishe ya kwamba kampuni ambazo hazisaidii chochote katika mazingira ya nchi hii zinawekwa katika orodha ya zile kampuni ambazo zinatakikana kufungwa. Nataka nichangie kuhusu afya ya akina mama wetu. Wakati walipokuja katika ile Kamati, nilihudhuria. Walilalamika wakasema ya kwamba wanashindwa kula hata chakula cha jioni wakati LDKL wanafungua ile mashine ambayo inatoa ile harufu mbaya. Ni lazima tuangalie ni nini muhimu katika nchi hii. Je, ni afya ama ni pesa ambazo LDK inapatia Serikali hii?"
}