GET /api/v0.1/hansard/entries/836918/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 836918,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836918/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "wafanyikazi wao ambao pia ni mabalozi wasaidizi wakimsaidia balozi mwenyewe ni kwamba pesa zile ambazo wanapatiwa hazitoshi miaka nenda miaka rudi. Ukiangalia Bajeti inavyopitishwa, ofisi ya ubalozi bado inapatiwa pesa kidogo kulingana na muda ambao umepita. Ukiangalia hesabu inayofanywa, hawajabadilisha pesa walizopeana miaka kadhaa iliyopita mpaka sasa hivi ilhali hela yetu ya Kenya imeshuka nguvu kufananisha na pesa za nje. Hivyo basi, inaonekana kuwa kuna upungufu mkubwa sana wa pesa za kufanya kazi ile ambayo waliotumwa kule nje. Suala la pahali ambapo ofisi zetu za ubalozi zipo pamoja na pale wafanyikazi wetu wanapokaa huko nchi za kigeni limekuwa suala nyeti na limezungumziwa kwa muda mrefu. Kuna wakati nakumbuka nikiwa waziri, waziri mwenzangu alifanya uamuzi wa kuuza sehemu fulani ambapo tulitakikana kujenga maeneo ya ubalozi na ikatutatiza sana wakati huo. Tulifikiria kuwa tungetafuta pesa kwenye Bajeti za kusaidia kujenga maeneo yale ili ubalozi wa Kenya uwe pahali pa hakika. Vile vile, ukiangalia maeneo mengine ambapo tunafanya shughuli nyingi kama vile nchi ya Uchina, ukienda kule mara nyingi Wakenya wengi wanafanya shughuli zao haswa za kibiashara upande wa Guangzhou lakini hawana ofisi ama ubalozi ambapo wanaweza kwenda kupata usaidizi. Vile vile, mara nyingi, eneo lile ambalo watu wanaweza kutumwa kushughulikia chochote, kuna umbali kana kwamba hata ukisafiri na ndege, ni masaa matatu na nusu mpaka Beijing ambapo ofisi zetu zipo. Hivyo basi nakubaliana na Kamati hii kuwa kuna umuhimu wa Serikali yetu kufungua ofisi ya ubalozi mara moja katika eneo la Guangzhou ili Wakenya walioko kule waweze kupata huduma na pia uhusiano wetu na nchi ile uimarike. Vile vile, ukienda kwenye ofisi za ubalozi, utakuta wana matatizo makubwa sana haswa kwenye masuala ya magari. Mara nyingi inawabidi watafute magari ya kukodisha. Magari ya kukodisha huwa ya bei ya juu. Kwa kifupi sana, ningependa kuzungumzia swala hili la sisi kulipa kodi ya nyumba kwenye maeneo yale. Bei ya kulipa iko juu hata kushinda bei ya kulipa deni kama tutakuwa tumechukua deni kwa uhusiano wetu na zile nchi na haswa benki zile ziko kule ili kuweza kujenga ubalozi kule nchi za nje. Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu, wale wengi waliojenga kwa mfano nchi ya Uganda na nchi zingine ambazo zina majumba, maeneo yale kama upande wa New York na London, utaona wanapata hela nyingi kiuchumi na zinatumika kwenye wizara ya kusimamia masuala ya nje ili kuimarisha shughuli za ubalozini. Maeneo yale ambayo yanahitaji ubalozi mdogo haswa maeneo kama yale niliyotaja kwa mfano Uchina na nchi zinginezo, pahali ambapo Wizara hii imeona kuna umuhimu wa kufungua maeneo yale, kuna umuhimu wa Bunge hili, na haswa Kamati inayohusika kushikana na kuzungumza na wizara pamoja na Rais wetu na Naibu wake ili kuhakikisha ya kwamba maeneo yale yanaweza kupatiwa ubalozi huu haraka iwezekanavyo."
}