GET /api/v0.1/hansard/entries/836919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 836919,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/836919/?format=api",
    "text_counter": 246,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono kazi hii ambayo imefanywa na Kamati hii lakini wasiiachie hapo. Waendelee na kuhakikisha ya kwamba masuala hayo waliyoyataja hapa, ambayo ni muhimu, yametekelezwa mara moja. Tunapokwenda kwenye mwaka ujao wa kutengeneza Bajeti inayokuja, tuangalie umuhimu wa kupatia pesa za kutosha masuala yaliyotajwa hapa, na haswa tuangalie kama hela hizo zinatosha ama hazitoshi kwa shughuli zile zinazoendelea na kuita wawekezaji. Ubalozi ndio unaweza kutuunganisha na nchi za nje ili kuhakikisha kuwa wawekezaji wamekuja kwa nchi yetu kwa wingi kufanya biashara huku na kufungua makampuni ambayo yatawapatia kazi watu wetu, na haswa vijana."
}