GET /api/v0.1/hansard/entries/837302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 837302,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/837302/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, asante kwa kunipa muda huu kuchangia Mswada huu unaohusu wazee. Kwanza, watu wazee ni baba, mama, nyanya na babu zetu. Nakumbuka nikiwa mdogo, nyanya yetu alikuwa mzee sana. Kazi yake ilikuwa kutuombea sisi watoto wa mtoto wake. Kwa hivyo, jukumu hili lingefaa kubakia kwa watoto, wajukuu na vitukuu. Hata hivyo, haiwezekani vile hali ilivyo. Mara kwa mara tunasikia habari za vifo vya ajuza ambao wametelekezwa. Watoto wao wa kike wanapoolewa, ajuza huwachwa peke yao. Wakati mwingine wao hubakwa na kunyofolewa sehemu zao za siri. Mswada huu utachangia pakubwa kuweka viwango vya makao ya wazee ambao ni mama, baba, nyanya na babu zetu. Tayari kuna makao ya wazee. Kule kwetu pwani, ukiita mtu mzee, atakwambia wazee wako Chuda kwa sababu kule kuna makao ya wazee. Iwapo mtu anataka kuanzisha makao ya wazee, kuna vigezo atakavyo takikana kuzingatia kabla ya kupewa fursa ya kuanzisha. Vile Sen. Cheruiyot amesema, sheria hii si ya wale wazee ambao wako peke yao bali hata sisi ambao saa hii ni vijana wenye nguvu lakini wakati utafika na tutakuwa wazee pia. Je, tukiwa wazee tungependa kuishi katika mazingira aina gani? Kule kwetu nilimuona mama mzee wa miaka 130 ambaye alikuwa hajiwezi. Hangeweza hata kugeuka. Watoto wake waliajiri kijakazi wa kumpeleka nje aote jua, kumpatia chakula na kumrejesha ndani ya nyumba jioni. Je, kama wale watoto hawakuwa na uwezo wa kumuajiri kijakazi, yule mama angeishi maisha ya aina gani?"
}