GET /api/v0.1/hansard/entries/837307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 837307,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/837307/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nimeona katika pitapita zangu mtaani mzee aliyekuwa na nguvu zake za kufanya kazi, lakini ametelekezwa na watoto wake. Kuna funza kwa miguu, mikono, tumbo hadi katika sehemu nyeti. Mswada huu utamsaidia mtu kama huyo ili aishi maisha ambayo ni ya kibinadamu. Itamuwezesha kuchangia katika maendeleo ya taifa letu la Kenya. Bi Spika wa Muda, tayari kuna miradi ambayo inaendelea ya kusaidia hawa wazee. Serikali Kuu inatenga kiasi kidogo cha fedha, labda Kshs2,000 au Kshs3,000 ya kuwapa wazee ambao wana zaidi ya miaka 70. Hata hivyo, pesa hizo haziwezi kumsaidia mama kupika chakula, kunua dawa, kuoga au kuajiri mjakazi. Kuna serikali za Kaunti ambazo zinatoa madawa ya bure kwa wazee. Hata hivyo, hata upewe dawa na hauna chakula pale nyumbani, yale maisha bado yatakuwa ni ya uchochole. Badala ya Serikali Kuu na serikali za gatuzi kupeana pesa katika njia ambayo haina mpangilio kamili, Mswada huu unaweza kusaidia pakubwa kutenga pesa ambazo zitapelekwa kwa nyumba za wazee na kuajiri watu ambao wana tajiriba au uwezo wa kuwatunza wazee ambao ni baba na mama wetu. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuwa na sheria ya kuangalia jinsi tutakavyowatunza wazee wetu. Namshukuru sana Sen.Cheruiyot kwa kuleta Mswada huu. Nilikuwa nataka kuanzisha nyumba ya watoto ambao ni walemavu, lakini nikaambiwa kwamba siku hizi zimesimamishwa. Niligundua kwamba hakuna sheria inayosimamia nyumba za watoto kama wale na pia nyumba za wazee. Kwa hivyo, hii sheria itatusaidia kuangalia maslahi ya wazee wetu tukikumbuka kwamba ni haki ya kikatiba kuishi maisha ambayo ni ya heshima na yanayoweza kuwasaidia kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu ya Kenya. Kuwatunza wazee wetu ni jambo ambalo liko katika Article 57 ya Katiba yetu. Tukipitisha Mswada huu ambao unaitwa “ The Care and Protection of the Older"
}