GET /api/v0.1/hansard/entries/837758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 837758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/837758/?format=api",
"text_counter": 389,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi. Ninataka kusisitiza zaidi kuhusu ujirani. Ukiwa na jirani mwema na mkiwa na mawasiliano mazuri, mnakaa vizuri hata wewe mwenyewe huwa unapata utulivu wa moyo. Ninahimiza sana huu ujirani na ushirikiano. Kusema kweli, tumetoka mbali kama jumuiya ya Africa Mashariki. Hapa tulipofika, wengi watakubaliana na mimi kwamba kulikuwa na matatizo mengi na tulianza pahali na saa hii tumefika pahali pazuri. Kuna mambo mazuri yanayopatikana upande wa usalama kwa sababu vile tunashirikiana kibiashara na tunafaidi. Ninataka kuhakikishia Bunge hili kwamba sisi Wakenya kwa ukarimu wetu, kama vile ulivyosema Bw. Spika, wewe ukiwa mkarimu sio lazima utarajie mwingine akulipe. Kwa hilo, mwenyezi Mungu anatubariki na ninawahakikishia kwamba tunafaidi kwa hilo. Nina hakika majirani zetu watakuja kuona. Hawako mbali kuja kuona kwamba sisi tunafaidi na wao watafungua njia. Mwanzo ningependa kumpongeza Rais kwa kutoa nafasi majirani waje bila kutumia pasipoti ila kitambulisho pekee. Hiyo imetufungulia biashara vizuri Kenya. Wameanza kuhisi. Wako karibu watakuja kuona. Wakiendelea kukaa mbali, sisi tutaendelea kufaidi. Sina mengi zaidi isipokuwa hayo tu. Ninawahakikishia Wakenya kwamba tukiwa wazuri tunafaidi. Mimi pia niko kwa hii Kamati na tumeuliza maswali na tumehakikishiwa kwamba tunafaidi. Hatuendi hasara. Asante."
}