GET /api/v0.1/hansard/entries/838488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 838488,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/838488/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii fursa. Ukweli wa mambo ni kwamba katiba hutengenezwa na binadamu. Binadamu pia hurekebishwa. Huwezi kuwa na sheria ambazo zinakunyonga halafu ubaki ukisema eti ni sheria au kwamba tumeweka Katiba na tukae tukiumia. Ni lazima tuangalie vile vipengele vinaumiza wananchi. Ni juzi tu tumepitisha masuala ya ushuru hapa. Tuliona kwamba wananchi walikuwa wanaumia. Ukiangalia kikatiba, serikali za wilaya zilipigwa marufuku na Katiba na sisi bado tunaendelea kuzishikilia. Hii ni kumaanisha Katiba ina taabu zake hapa na pale. Kwa kawaida, Wakenya huwa wanapumzika msimu wa Desemba ama mwezi wa kumi na mbili. Mmesikia Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) wakisema kwamba wanataka kuondoa maeneo ya Bunge. Kisa na maana ni kwamba Wakenya wengi mahali kama kule kwangu Mwatate, hatuna kiwanda chochote. Kwa hiyo, ni lazima watu wafanye kazi Nairobi. Lakini, hizi kura zikiwekwa mwezi wa kumi na mbili, wengi watatoka hapa na watapiga kura. Tutakuwa tumefikia kile kiwango IEBC wanataka. Kwa hivi sasa, mimi kama mwalimu, ukiangalia mitihani iliyofanywa mwaka jana, watoto wengi hawakujiandaa sawasawa. Kura zilipokuwa zinapigwa Agosti, watoto wengi hawakujiandaa sawasawa. Hili swala liko kwa wananchi wote wa Kenya. Wanajiuliza, hata ukienda mitaani utasikia wakiongea."
}