GET /api/v0.1/hansard/entries/838568/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 838568,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/838568/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "kwa Hoja hii. Ni kweli vijana wetu wengi hawajaajiriwa. Kulingana na utafiti wa United Nations Development Programme (UNDP), asilimia 39 ya vijana wa Kenya hawajaajiriwa. Ukipima, hicho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na majirani wetu kama Tanzania, Uganda na wengine. Nawakilisha Kaunti ya Lamu. Kenya National Bureau of Statistics walisema asilimia 68 ya vijana wetu hawajaajiriwa. Ni kiwango kikubwa sana. Kutoajiriwa huleta uhalifu. Kwa mfano, utaona ya kwamba kaunti nyingi ambazo watu hawajaajiriwa, uhalifu uko juu zaidi. Mfano ni Lamu ambapo uhalifu uko juu zaidi. Vijana wetu wameingia kwenye mihadarati sana. Hii inachangia matatizo zaidi. Kwa mfano, ugonjwa wa ukimwi umekuwa juu zaidi. Ugonjwa huu na mihadarati ni janga kubwa katika Kaunti ya Lamu. Tunapambana na mihadarati. Tunapeleka vijana waende wakajikomboe na mihadarati lakini wakirudi wanarejelea. Kwa hivyo, kukosa kazi kwa vijana wetu kumechangia shida nyingi."
}