GET /api/v0.1/hansard/entries/838569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 838569,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/838569/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Serikali pia kwa mipango yake saa zingine husababisha watu kukosa kazi zaidi. Kwa mfano, katika Kaunti ya Lamu, wakati Lamu Port -South Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor Project ilipoanza, wavuvi wengi hawangeweza kwenda baharini. Kwa hivyo, imechangia ukosefu wa ajira. Kuna kiwanda ambacho kinataka kuwekwa cha makaa. Sehemu hiyo ilikuwa na wakulima ambao walikuwa wamekaa hapo miaka mitatu wakingojea walipwe. Hawalimi sasa. Hii imeleta ukosefu wa ajira na wengi ni vijana. Pia kuna mpangilio wa Serikali uliyowekwa wa kutokata mikoko. Hii imechangia pakubwa ukosefu wa ajira kwa familia 3,000 katika Kaunti ya Lamu. Mipango hii ambayo iko katika Hoja hii itasaidia pakubwa."
}