GET /api/v0.1/hansard/entries/839014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839014/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili nijiunge na Maseneta wenzangu kulipongeza Bunge la Seneti na Karani wetu kwa vikao vyema ambavyo tulifanya mjini Eldoret. Vile vile, ninachukua fursa hii kumpongeza Sen. (Prof.) Kamar, Seneta wa Kaunti ya Uasin Gishu kwa makaribisho na kututunza vizuri kwa muda was siku tano. Ilikuwa ni tajriba nzuri kwa sisi ambao tunahudumia Seneti kwa mara ya kwanza, kwa sababu tumepata fursa ya kuonana na wananchi wengine wa Kenya ambao labda hatungeweza kuwaona katika kazi zetu za kawaida. Sio wengi wanaopata fursa kuja hapa kulitembelea Bunge la Seneti. Kwa hivyo, safari zetu katika eneo la Eldoret zisiwe za mwisho. Tutembelee kaunti zingine. Kama Seneta wa Mombasa, ninachukua fursa hii kuwaalika Mombasa. Wakati wowote mkiwa tayari tutawapokea. Mwisho, tumesoma mambo mengi ambayo yanafanyika katika sehemu tofauti. Kwa mfano, tuliweza kusikiza petition ya wakaazi wa Kericho kuhusiana na ile ardhi ambayo ilichukuliwa na multinationals hapo nyuma. Tatizo hili liko katika Kaunti jirani ya Nandi na pia kaunti nyingi zina matatizo kama haya. Kwa hivyo, haya ni mambo ambayo lazima Bunge la Seneti likae, tuyatatue haraka ili wananchi wawe na matumaini kwamba sisi twaweza kuyatatua matatizo ya nchi ya Kenya. Asante Bw. Spika. Mungu akubariki."
}