GET /api/v0.1/hansard/entries/839238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839238/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "ni lazima kuwe na mashtaka ambayo yanaweza kuwa na uzito fulani. Tunajua kuwa CECs katika kaunti zetu wanajiita mawaziri. Sijui ni kwa sababu gani hatujaweza kuchukua hatua kwa jambo kama hili. Tukienda katika mikutano mbalimbali, hawa hujiita mawaziri. Sisi tunajua Waziri ni yule anayechaguliwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Kenya. Mhe. Naibu Spika, kando na hayo, tunajua kuwa mashtaka au madai ya kuweza kumwondoa kiongozi kutoka mamlaka kama hayo niliyotaja ni lazima kuwe na mashtaka ambayo yanaweza kuwa na uzito fulani. Mswada huu ni muhimu sana kwa sababu katika Bunge lililopita mimi nilikuwa mmoja wa Maseneta ambao tulijishughulisha na mashtaka dhidi ya kumwachishwa kazi kwa Gavana wa wa Kaunti ya Murang’a, mhe. Mwangi wa Iria. Hatimaye hatukuweza kufaulu kwa sababu alikimbia kortini. Korti ikatoa uamuzi wa kusimamisha Bunge kufanya kazi yake juu ya gavana huyo. Sisi Wabunge tuliochaguliwa tukiwa na majukumu kama haya, sheria hii ni mwafaka sana kwa wakati huu. Tunajua kumekuwa na viongozi ambao wamekuwa wakizembea kazi baada ya kupewa nyadhifa na kimbilio lao kubwa limekuwa kortini. Tunasema Mswada huu uwezekufafanua vyema kwamba kukiwa na shughuli za The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}