GET /api/v0.1/hansard/entries/839241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839241,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839241/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kumwachisha kazi mfanyikazi wa Serikali, korti isimame kwanza, ingojee mpaka hatua ya Bunge la Seneti imalizike. Wakati huo sasa mtu anaweza kupewa nafasi ya kwenda kwingine kufanya juhudi kama vile kusimamisha kesi hiyo. Mhe. Naibu Spika, kwa maoni yangu Mswada huu umelenga hasa zaidi upande ule ambao watu wataku wawanavunja sheria. Kuna njia mbili za uvunjaji wa sheria: kwanza, uvunjaji wa sheria mtu akiwa bado ofisini na nje ya ofisi. Wale wanaopewa nafasi kama hizi wanafanya mashirika tofautitofauti ya Serikali. Kumekuwa na uvunjaji wa sheria. Tunasema ya kwamba sheria hii inawezakufafanua hayo zaidi. Ingeweza kuleta mambo tofautitofauti lakini tunasema ya kwamba muda uliopewa siku 30 kufanya shughuli hii ndani ya Bunge nimwafaka kabisa. Utakubaliana na mimi kuhusu nafasi ya siku 30. Mimi kama wakili naona kuwa mtu anawezakujitetea vilivyo kwa muda ya siku 30. Naona kuwa muda ambao tumeweka ukipunguzwa itakuwa jambo bora zaidi katika sheria hii ikiwaitapitishwa hapa. Mhe. Naibu Spika, mwisho, nasisitiza ya kwamba fitina ni kigezo kibaya. Mara nyingi tunaona ya kwamba magavana wamekuwa wakifanya kazi katika kaunti zao aidha wakiogopa mamlaka ambayo yana Wabunge Wa Kaunti (MCAs) ya kuweza kuchukua hatua kama hii. Gavana pia anaweza kukubaliana nao ili awezekujiokoa na aendelee na kazi. Nasema hivi kwa sababu tunapata kwamba wakati mwingi wale MCAs wakati ule ilikuwa kuanzisha shtaka kama hili ni lazima kwanza wamwambie gavana kuwa asipofanya kitendo fulani, basi wangechukua hatua fulani. Hayo yalikuwa mambo ya fitina. Mswada huu umefutilia bali mambo ya fitina. Ni lazima kuwe na mambo kamili katika mashtaka ya kumsimamisha mfanyikazi wa Serikali. Asante, Mhe. Naibu Spika."
}