GET /api/v0.1/hansard/entries/839486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 839486,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839486/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ahsante, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ombi ambalo limeletwa la kuwalipa ridhaa wale ambao wameathirika na bypass . Ni kweli kwamba serikali inazembea katika kulipa wale wanaoathirika na miradi ya maendeleo ya serikali. Tuko na mfano wa SGR kule Mombasa ambapo watu zaidi ya 76 hawajalipwa. Hii ni kuanzia kilomita zero hadi 20. NLC ililipa mashirika matatu Shilingi Bilioni tatu na nusu na wakaacha walalahoi karibu 70 bila malipo yoyote. Tuliuliza swali hili katika Bunge la Senate lakini halijashughulikiwa mpaka leo. Wananchi bado wanalalamika ya kwamba hawajalipwa pesa zao. Ni muhimu ya kwamba watu lazima walipwe na serikali inapochukua ardhi kabla hawajaingia katika ardhi na kuanzisha miradi. Hii ni kwa sababu wengi wanaotakikana kulipwa ni walalahoi na wakiambiwa wavunje nyumba zao, hawajui watakapokwenda kuishi. Naunga Ombi hili mkono na ni lazima walipwe ndio waondoke. Mradi usiendelee mpaka walipwe ndio waondoke. Asante."
}