GET /api/v0.1/hansard/entries/839503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839503,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839503/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza ni kuwapa heko wale ambao wameleta maswala haya mbele ya Bunge la Seneti. Hawa watu wana uchungu mwingi sana kwa vile ardhi yao ilitwaliwa bila fidia yoyote au kufanyiwa haki. Wengi wao wanaambiwa watimuliwe kutoka kwa mashamba yao bila haki yao kutekelezwa. Matukio haya yanaendelea katika nchi nzima. Tumeona watu wakitimuliwa kutoka kwa mashamba yao bila kulipwa chochote. Tumeshuhudia haya yakifanyika katika Kaunti ya Kilifi. Nina uchungu sana kwa sababu watu wetu wametimuliwa kutoka mashamba yao bila malipo yoyote. Matajiri wana weka ua bila kujali kama kuna makao, vijiji, Misiki na makaburi. Wanatumia mashine makubwa makubwa kama vile greda kutoa miili ya watu wetu bila heshima. Ikiwa kuna mradi wanaotaka kuanzisha, basi ni vyema kuwahusisha watu wa sehemu hiyo na lazima walipwe ridha zao ili waweze kuondoka. Tuliona vile walianzisha mradi wa SGR na vile watu wetu sehemu za Mombasa na kwingineko wanendelea kuteseka. Ndugu yangu, Mhe. Faki amesema watu hawa hawajalipwa fidia au pesa zozote. Ni muhimu kwa Bunge la Seneti kuangaliwa swala hili kwa makini sana."
}