GET /api/v0.1/hansard/entries/839670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839670,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839670/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Prof.) Kamar kwa Hoja hii ambayo ameileta mbele ya Bunge la Seneti. Hoja hii imekuja kwa wakati mwafaka kwa sababu katika maeneo mengi ya nchi yetu kuna vijana wengi ambao hawana kazi baada ya kumaliza masomo yao ya darasa la nane na kidato cha nne. Kwa hivyo, Hoja hii imekuja kwa wakati mwafaka kwa sababu ni fursa nzuri ya kuweza kupanga hivi vyuo vya ufundi ili kusaidia wanafunzi ambao wanashindwa kuendelea na masomo yao. Nikizungumzia Kaunti ya Mombasa, zamani kulikuwa na shule ambayo ilikuwa inaitwa Magalal na ilikuwa ikifunza mambo ya kiufundi; ushonaji nguo, useremala, uashi, fundi wa umeme, na kadhalika. Wale wanafunzi walikuwa wanashona sare kwa wafanyikazi wa Mansipaa ya Mombasa. Vyuo kama hivi vitatumiwa zaidi si kuwafundisha wanafunzi tu lakini pia kuwapatia ajira wale wanafunzi wanaofanya masomo katika vyuo vile ili wanapoondoka wanapata ujuzi na biashara ya kuendeleza maisha yao. Jambo muhimu ningependa kusisitiza katika vyuo hivi ni kwamba lazima kuwe na ushauri, yaani mentorship. Vijana wengi wanaotoka katika vyuo vya ufundi na vyuo vikuu hawajapata ushauri wa kutosha vile watakavyoendesha kazi katika maisha yao mapya. Ni lazima tuwape ushauri wanafunzi wote; iwapo ni mwanafunzi wa uzamili, wa vyuo vidogo vya ufundi, wa hadhi ya diploma ama certificate. Hili linafaa kuwaonyesha ni vipi wataendesha kazi na biashara zao. Vile vile katika vyuo hivi, lazima kuwe na somo la ujasiriamali, yaani"
}