GET /api/v0.1/hansard/entries/839672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839672,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839672/?format=api",
"text_counter": 362,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ikiwa mwanafunzi atafuzu bila ujuzi wa ujasiriamali, ina maana kwamba atategemea kuajiriwa miaka nenda, miaka rudi. Itavunja ule ujuzi ambao amepata pale kwa sababu hawezi kujiajiiri mwenyewe. Kwa hivyo, mambo mawili ningeomba yafundishwe katika vyuo hivi ni kwamba lazima kuwe na kitengo cha masomo ya ujasiriamali, enterprenuership na pia ushauri yani mentorship katika masomo ili mwanafunzi akitoka pale awe ni mwanafunzi kamili. Sehemu nyingi katika Jamhuri yetu ya Kenya, mwanafunzi anapomaliza darasa la nane anaachwa pekee ili ulimwengu umfundishe. Labda kuna sehemu zingine ambazo watu wameendelea kidogo; wanafundisha wanafunzi kazi ya useremela na mechanic . Lakini katika sehemu nyingi wanaachwa bila kazi. Inakuwa rahisi kuwaingisha wanafunzi kama hao katika itikadi kali, madawa ya kulevya na uhalifu. Hoja hii inafaa kuungwa mkono ijapokuwa kuanzisha vyuo vya ufundi katika kila wadi itakuwa vigumu kwa sasa kwa sababu kwanza Serikali za kaunti zina upungufu wa fedha. Pili, Serikali kuu pia haiwezi kuthamini mambo kama haya lakini inafaa kuanzia katika kila sehemu ya uakilishi Bunge tuwe na chuo kimoja cha kiufundi. Labda wakati huu itakuwa vigumu kufanya hivyo kwa sababu ya hali ya uchumi. Ni lazima tuanzishe vyuo hivi kwa sababu wanafunzi hawatapata elimu katika taasisi zingine. Watapata ujuzi katika vyuo vya kiufundi. Upungufu wa teknolojia umekuwa mkubwa sana kiasi ambacho zile nchi ambazo zimeendelea zimetuacha sana. Vyuo vya kiufundi kama hivi vitasaidia kuleta teknolojia karibu; iwapo ni ya ukulima, useremela, ufundi umeme na ufundi wa kila aina. Itakuwa rahisi kuleta ile teknologia mpya katika nchi yetu iwapo tutaweza kufanya vyuo vya kiufundi kama hivi . Kwa kumalizia ningependa kumpongeza Seneta wa Uasin Gishu, Sen. (Prof.) Kamar, kwa makaribisho murwa aliotupa kutoka tulipoingia hapa Jumanne na mpaka The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}