GET /api/v0.1/hansard/entries/839964/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 839964,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/839964/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "zamani ukanda wa pwani, yaani kaunti za Taita Taveta, Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu na Tana River hakuna uwanja wowote wanaweza kufanyiai mazoezi na kuendeleza michezo ya kimataifa. Aid mchezo wa kandanda, riadha, rugby, magongo ama chochote kile hakiwezi kufanyika kwa sababu hatuna uwanja ambao wanatumia kufanya mazoezi. Tunaelewa kuwa michezo na mambo ya vijana yamegatuliwa kwa serikali za kaunti. Hii ni fursa nzuri kwa serikali za ugatuzi kutenga kiwango fulani cha bajeti zao kwa ajili ya kuekeza katika viwanja vya michezo na mambo mengine ili kuinua michezo katika kila kaunti. Juzi, nilifurahi wakati tulipokuwa katika michezo ya KICOSCA kule Kisii nilimwona mchezaji wa zamani wa Shabana, Bw. Henry Motego, ameteuliwa kama afisa wa michezo katika Serikali ya Kaunti ya Kisii. Hiyo ni jambo nzuri kwa sababu tunajaribu kutambua talanta ambazo wako nazo wanamichezo wa zamani. Bw. Naibu Spika, michezo ni fedha hivi sasa kwa sababu tukiangalia wanamichezo wengi ambao wamefaulu katika mbio tofauti tofauti hapa Eldoret na kwingineko, ni watu ambao wamepata fedha nyingi na wanaekeza katika sehemu wanazotoka. Kwa hivyo, ni lazima serikali za kaunti zihakikishe kwamba zimetengeneza sehemu ambazo vijana wataweza kufundishwa michezo ili kuendeleza talanta zao katika michezo mbalimbali. Mwisho, Bw. Naibu Spika, michezo inaweza kusaidia nchi kuleta uwiano. Hivi sasa, kwa mfano, Joe Kadenge akitembea katika barabara za Mombasa, kila mtu anajua kwamba huyu ni Joe Kadenge, hawajali kwamba anatoka sehemu gani lakini wanakumbuka kwamba alikuwa mwanamichezo, alikuwa mwanakandanda mzuri. Kwa hivyo, tunaweza kutumia michezo yetu kuleta uwiano. Hasa maeno ambapo kuna mapigano ya kikabila. Inafaa michezo ipelekwe kule ili watu washindane kwa njia ya sawa sawa. Mwisho Mheshimiwa Spika, ningependa kumkumbusha Seneta Zawadi kwamba siku hizi hata kina dada wanamatawi, sio wanaume pekee ambao wanamatawi, hata kina dada pia wanamatawi. Asante, Bw. Naibu Spika."
}